Jarida la Forbes ambalo mara kwa mara
huwa linatoa Orodha ya watu
waliofanikiwa sehemu mbali mbali za
Dunia, limetoa Orodha ya watu 40
matajiri zaidi barani Afrika. Katika
Orodha hiyo Mtanzania pekee
aliyetokea ndio inaaminika ndio tajiri
kuliko wote Tanzania .
Said Salim Bakhresa ambaye
amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri
40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri
unaofikia Dollar milioni 520 hadi kufikia
November, 2012 .
Inaaminika kwamba Bakhresa aliachaga
shule akiwa na umri wa miaka 14 na
kujiingiza kwenye biashara ndogo
ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na
biashara ya unga wa kusaga. Leo hii
Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu
2, 000 na ni kampuni kubwa zaidi
Tanzania.
Bidhaa maarufu zile za Azam ambazo
zinajumuisha unga, vinywaji, ice cream
pia usafiri wa meli za mafuta miongoni
mwa nyingine.