Jumuiya Ya Uamsho na
Mihadhara Ya Kiislamu Zanzibar
.....
Amesema kuwa waliomchukuwa
walijitambulisha kwake kuwa ni
askari polisi na kumonesha
vitambulisho huku wengine
wawili wakiwa na silaha za
mshingani hapo hapo
wakamfunga macho yake kwa
kutumia kitambaa ili asijue wapi
anapelekwa walimchukua kwa
gari na baadae kumuingiza katika
nyumba asioijua kwa mahojiano
bila ya kumfungua kitambaa
hicho kwa muda ...
wa siku tatu mfululizo.
Amesema kuwa watu hao
waliomuhoji maswala mengi
sana kuhusu tangu kuuanzishwa
kwa jumuia ya uamsho na safari
zake za kwenda omani na mpaka
kumchukulia simu yake bila ya
kumrejeshea pia wametaka kujua
kuwa anauhusiano gani na rais
shein na makamo wakwanza wa
raisi maalim seif, wakati
wanamuhoji walifika mpaka
kupiga risasi chini ya miguu nyake
ili kumtisha na kuweza kufikia
lengo lao walilojipangia.
Amesema pia watu
waliomchukuwa na baadhi ya
waliokuwa wanamlinda hawezi
kuwajua kutokana na kuwa
walikuwa wamevaa soksi ndani ya
nyuso zao nakubakisha macho
tu,amsema kutokana tu na lafdhi
zao ambazo walikuwa
wanaongea inaonekana wazi
kuwa wengi ni kutoka bara na
wazanzibari ni kama wawili tu
kutokana na sauti zao.
kuhusu suala lakupigiwa simu na
mtu asiemjua amesena kuwa
wao kama viongozi huwa mara
nyingi wamekuwa wakipigiwa
simu na watu wasiowajua na
wamekuwa wakionanan nao bila
ya matatizo hivyo basi kitendo
cha kupigiwa simu siku hio na
mtu asiemjua hakikumshituwwa
kwani nikawaida kwao hususani
aliemnigia alijitambulisha kama ni
mwanafunzi wake wa mahad
lmahfudh
Aidha amesema kuwa muda
wote huo wa siku tatu hakuweza
kula chochote katika chumba
hicho kwani alikuwa hawaamini
na badala yake alikuwa
anakunywa maji kutoka bomba la
mfereji lililokuwa chooni katika
chumba hicho pia amesema
wakati yupo ndani hakujua lolote
linaloendelea huku nje isipokuwa
amejua baada ya kutoka nje kwa
kuambiwa na kila manaemkuta.
Aidha sheikh farid ameiomba
serikali ya mapinduzi ya zanzibar
kutumuia sheria na uadilifu kwa
rai wake kinyume cha hivo
watakuwa wanaimba tu katika
nchi amani na utulivu
usiokuwepo pia amewataka
wazanzibar kuendelea kutetea
maslahi ya nchi yao kama
kawaida kwani kufanya hivo ni
haki yao na yeye amewahakikishi
ataendelea kuitetea zanzibar
mpaka tone la mwisho la damu
yae.
Saturday, October 20, 2012
HUU NDO MKASA MZIMA WA KUTEKWA KWA SHEIKH FARIDI.
Thursday, October 18, 2012
HAYA NDO MATOKEO YA MJADALA KATI WA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA NA MGOMEA WA URAIS MITT ROMNEY
Kituo cha Tv cha CNN kilitoa majibu
ya maswali yaliyoulizwa kwa
watazamaji wa mjadala wa Rais
Obama wa Marekani na Mitt
Romney , waliotazama walipiga kura
na matokeo ni haya hapa chini .
Nani amependwa zaidi? Obama
asilimia 47 Romney 41.
Nani amemshambulia mwenzake
zaidi? 49% Obama Romney 35%
Nani alionekana kuwajali zaidi
waliokuwa wakifuatilia Obama 44%
Romney 40%
Nani alijibu vizuri bila
kukwepakwepa maswali? Obama
45% Romney 43%
Nani anaweza kudhibiti hali ya
uchumi vizuri zaidi? Obama 40%
Romney 58%
Nani ana sera nzuri zaidi za afya?
Romney 49% Obama 46%
Nani ana sera nzuri zaidi za ushuru
na mapato? Romney 51% Obama
44%
Nana anaweza kuthibiti madeni ya
nje bora zaidi? Romney 59% Obama
36%
Nani ana sera bora kwa uhusiano na
nchi za nje? Romney 47% Obama
49%
Romney ana sera bora kutatua
matatizo yanayoikabili nchi?
Waliosema ndio ni asilimia 49,
Hapana 51%.
HAYA NDO MATOKEO YA MJADALA KATI WA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA NA MGOMEA WA URAIS MITT ROMNEY
Kituo cha Tv cha CNN kilitoa majibu
ya maswali yaliyoulizwa kwa
watazamaji wa mjadala wa Rais
Obama wa Marekani na Mitt
Romney , waliotazama walipiga kura
na matokeo ni haya hapa chini .
Nani amependwa zaidi? Obama
asilimia 47 Romney 41.
Nani amemshambulia mwenzake
zaidi? 49% Obama Romney 35%
Nani alionekana kuwajali zaidi
waliokuwa wakifuatilia Obama 44%
Romney 40%
Nani alijibu vizuri bila
kukwepakwepa maswali? Obama
45% Romney 43%
Nani anaweza kudhibiti hali ya
uchumi vizuri zaidi? Obama 40%
Romney 58%
Nani ana sera nzuri zaidi za afya?
Romney 49% Obama 46%
Nani ana sera nzuri zaidi za ushuru
na mapato? Romney 51% Obama
44%
Nana anaweza kuthibiti madeni ya
nje bora zaidi? Romney 59% Obama
36%
Nani ana sera bora kwa uhusiano na
nchi za nje? Romney 47% Obama
49%
Romney ana sera bora kutatua
matatizo yanayoikabili nchi?
Waliosema ndio ni asilimia 49,
Hapana 51%.
Wednesday, October 17, 2012
WAISLAM ZANZIBAR WAKINUKISHA
HIZ NDO PICHA ZIKIONESHA JINS GANI HALI ILIVYOKUA SI SWARI HUKO ZANZIBAR..
Inasemekana ni kikundi cha waislam cha UAMSHO kilikua kinaandamana kikihitaji kuachiwa huru kwa kiongozi wao aliyekamatwa na polisi na kuwekwa ndani na sasa hali si shwari maeneo ya darajani.. Kiongozi wa Kundi
linaloitwa UAMSHO la Zanzibar
Sheikh Farid aliyekamatwa huko
Visiwani Zanzibar ndo anayesababisha vurugu zote huko. kama ujui basi UAMISHO ni Kundi la kiislam na shughuli zake ni za mihadhara ya
Kidini hasa ya Kiislam.
HAYA NDO MATOKEO YA MECHI ZA JANA
World Cup qual.
Europe (Group A)
01:41October 16
FT Croatia 2 - 0 Wales
FT Rep. of Macedonia 1 - 0 Serbia
FT Belgium 2 - 0 Scotland
World Cup qual.
Europe (Group B)
October 16
FT Czech Republic 0 - 0 Bulgaria
FT Italy 3 - 1 Denmark
World Cup qual.
Europe (Group C)
October 16
FT Faroe Islands 1 - 4 Rep. of Ireland
FT Austria 4 - 0 Kazakhstan
FT Germany 4 - 4 Sweden
World Cup qual.
Europe (Group D)
October 16
FT Andorra 0 - 1 Estonia
FT Romania 1 - 4 Holland
FT Hungary 3 - 1 Turkey
World Cup qual.
Europe (Group E)
October 16
FT Cyprus 1 - 3 Norway
FT Iceland 0 - 2 Switzerland
FT Albania 1 - 0 Slovenia
World Cup qual.
Europe (Group F)
October 16
FT Russia 1 - 0 Azerbaijan
FT Israel 3 - 0 Luxembourg
FT Portugal 1 - 1 Northern Ireland
World Cup qual.
Europe (Group G)
October 16
FT Latvia 2 - 0 Liechtenstein
FT Bosnia-Herzegovina 3 - 0 Lithuania
FT Slovakia 0 - 1 Greece
World Cup qual.
Europe (Group H)
October 16
FT Ukraine 0 - 1 Montenegro
FT San Marino 0 - 2 Moldova
Postp. Poland ? - ? England
World Cup qual.
Europe (Group I)
October 16
FT Belarus 2 - 0 Georgia
FT Spain 1 - 1 France
World Cup qual.
South America
20:41 October 16
FT Bolivia 4 - 1 Uruguay
World Cup qual.
Asia (Group 1)
October 16
FT Qatar 0 - 1 Uzbekistan
08:41 October 17
FT Iran 1 - 0 Korea Republic
World Cup qual.
Asia (Group 2)
October 16
FT Oman 2 - 1 Jordan
FT Iraq 1 - 2 Australia
HIKI NDO KILICHOSABABISHA KIFO CHA YULE KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA MWANZA
YADAIWA NI KISASI CHA
MAPENZI, MTUHUMIWA
ATIWA MBARONI, DK BILAL
AONGOZA WAOMBOLEZAJI
DAR
Waandishi Wetu MWELEKEO wa upelelezi wa mauaji ya aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow umebadilika na sasa tukio hilo linahusishwa na kisasi cha mapenzi na tayari mtu mmoja anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi Mwalimu Dorothy Moses kutiwa mbaroni na
polisi.Awali, ilidaiwa kwamba Kamanda Barlow ambaye aliuawa kwa risasi usiku wa kuamkia Jumamosi muda mfupi baada ya kumfikisha mwalimu huyo nyumbani kwake, alivamiwa
na majambazi.
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, DCI, Robert Manumba alithibitisha jana kukamatwa kwa mtu huyo (jina tulihifadhi) akisema: "Ni kweli mtu mmoja
amekamatwa, lakini kwa
sasa siwezi kuzungumzia
kwa kina kuhusu suala hilo kwa sababu bado tunamhoji na tunaendelea na uchunguzi.
Tutakapokamilisha, tutatoa
taarifa." Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lily Matola pia alithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo. Hata hivyo, alisema
amesikia habari hizo kwa kuwa yuko safarini kwenda mkoani Kilimanjaro kwenye mazishi ya kamanda huyo...
"Hayo nimesikia, lakini kwa sasa sipo Mwanza hivyo siwezi kuzungumzia lolote."
Habari za uhakika kutoka ndani ya
Jeshi la Polisi, zinaeleza kwamba
upelelezi wa mauaji hayo
umefanikiwa kwa hatua kubwa na
kwamba mtu huyo alikamatwa Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego na makachero waliopo katika timu ya
uchunguzi na alisafirishwa hadi
Mwanza ambako anashikiliwa na jeshi hilo.
Ilielezwa kuwa mtu huyo alikamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa za siri za kiitelejensia kutoka kwa watu mbalimbali.
"Kuna hali imefunguka na imesaidia sana. Inaonyesha kwamba Dorothy alikuwa na uhusiano na mtu huyu ambaye alikuwa akifika nyumbani
kwake, kama mumewe na watu
wanajua jambo hili," alieleza mmoja wa askari polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Alisema kwamba uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba uamuzi wa mwalimu huyo kusitisha uhusiano wa mapenzi na mtu huyo huenda ndicho
chanzo cha mauaji hayo lengo likiwa ni kumshawishi Dorothy kurejesha uhusiano.
"Mimi natambua kwamba huyu jamaa na Dorothy walikuwa na uhusiano na inajulikana mjini kuwa hata mke wa mtuhumiwa anatambua jambo hilo
kwani walishagombana siku moja
mjini na hata katika msiba nyumbani kwao na mtuhumiwa," alisema mama mmoja (jina tunalo), aliyejitambulisha
kama mmoja wa marafiki wa karibu wa Dorothy.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitangiri (jina tunalo), anasema amekuwa akimfahamu mtuhumiwa aliyekamatwa kama baba mwenye nyumba hiyo na kila mara amekuwa akimkuta hapo nyumbani wakati wa
kujisomea na wanafunzi wenzake.
"Mimi ninamfahamu kama baba wa rafiki yangu na nimewahi kumkuta wakati wa kujisomea hapo nyumbani na watoto wa nyumba hiyo."
Dorothy ambaye ametajwa kuwa
mjane, ni Mwalimu katika Shule ya
Msingi Nyamagana na tangu kufariki
kwa mumewe Ofisa wa zamani wa
TRA, Modest Lyimo mwaka 1997.
"Watu wote wanajua kwamba
mtuhumiwa alikuwa akitembea na
huyo mwalimu, wameonekana mara
nyingi wakiwa muziki," alieleza mmoja
wa ndugu wa karibu wa mke wa
mtuhumiwa.
Hili ni tukio la tatu mkoani Mwanza
kutokea kwa ofisa wa polisi kuuawa.
Katika tukio la awali lililotokea mwaka
1987, askari aliyetambulika kwa jina la
Inspekta Gamba aliuawa kwa risasi na
watu wanaosadikiwa kuwa ni
majambazi eneo la Nyakato na katika
tukio la pili mwaka 1997, aliyekuwa
Mkuu wa Kituo cha Kati ASP Mahende
aliuawa kwa kupigwa risasi eneo la
Bugando saa nne usiku alipokuwa
akifuatilia majambazi waliokuwa
wakijitayarisha kuvamia.
Dar wamuaga Kamanda Barlow
Makamu wa Rais, Dk Mohamed
Gharib Bilal aliongoza waombolezaji
waliofika kutoa heshima za mwisho
kwa mwili wa marehemu Barlow
nyumbani kwake, Ukonga Dar es
Salaam jana.
Mwili wa Kamanda Barlow ambao
unasafirishwa leo kwenda mkoani
Kilimanjaro kwa mazishi, uliwasili
nyumbani kwake saa 6.45 kabla ya
kupelekwa katika Kanisa la Mtakatifu
Agustino, Ukonga kwa ajili ya ibada na
kutoa heshima za mwisho.
Akitoa salamu za Serikali, Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Silima alisema kifo cha Kamanda
Barlow ni pengo kwa taifa...
"Tutahakikisha watuhumiwa
wanapatikana kwa mikono yote miwili
na hatua za kisheria zinachukuliwa
dhidi yao."
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said
Mwema alisema juhudi za kuwasaka
watuhumiwa zinaendelea kwa
ushirikianao wa wananchi.
"Kifo cha Kamanda Barlow kimeacha
pengo kwani hivi sasa askari mmoja
analinda watu 1,300 hivyo kwa kifo
chake unaweza kuona ni pengo la
aina gani na ukilinganisha yeye
alikuwa kamanda wa mkoa mzima,"
alisema IGP Mwema.
Alisema jeshi lake litaendelea kulinda
amani ya wananchi na kifo cha
Kamanda Barlow kinalifanya liongeze
nguvu.
Akitoa mahubiri, Padri Veri Urio
alisema kila jambo hutokea kwa wakati
na kifo cha Kamanda Barlow
kimesababishwa na watu. Alisema
mwenye mamlaka ya kuondoa uhai
wa mtu ni Mungu pekee hivyo
waliosababisha kifo chake siku ikifika,
watajibu kwa nini walifanya hivyo.
IGP Mstaafu, Omary Mahita alisema
atamkumbuka Kamanda Barlow kwa
uchapaji wake kazi tangu akiwa polisi
Interpol (polisi kimataifa)alifanya kazi
kwa weledi uliotukuka.
"Daima nitamkumbuka kwani
nimefanya naye kazi sehemu tofauti
na askari waliobaki waige mfano wake
wa uwajibikaji" alisema Mahita.
Mbali ya Dk Bilal, viongozi wengine
walioshiriki katika ibada hiyo jana ni
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Meck Sadiki, makamanda wa
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),
makamanda wa polisi, viongozi wa
Serikali na vyama vya siasa na
wananchi.
Tuesday, October 16, 2012
I PHONE 5 ZAGOMBANIWA KAMA NJUNGU DAR ES SALAAM
Ule usemi wakuwa kama we ni masikini basi masikini peke yako Umethihirika baada Wakala ambae anahusika na mauzo
ya vifaa vya Apple Dar es salaam
Tanzania (Elite Computers)
amethibitisha kwamba simu 10
mpya aina ya iPHONE5 alizozileta
Tanzania wiki iliyopita
zimenunuliwa zote.
Simu moja ilikua inauzwa kwa dola za kimarekani 1350 ambazo kwa Tanzania ni zaidi ya milioni mbili.
Inasemekana wanunuz wengi wa simu hizo ni
wafanyabiashara, na inasemekana
mpaka sasa kuna watu mbalimbali
wakiwemo mawaziri kadhaa wa
Tanzania ambao wametoa oda
zikiletwa nyingine waambiwe.
Wakala amesema waliamua kuleta hizo simu chache kwa sababu walijua zingechukua muda mrefu kununuliwa, yani hawakudhani kama simu 10 zingeweza kununuliwa ndani ya wiki moja manake hata iPHONE 4s kwenye wiki yake ya kwanza Dar es salaam hazikununuliwa kwa wingi kama
hivyo.
HII IMETOKEA UGANDA, KIBABA KIMEJIFANYA WAZIRI WA MAMBO YA NJE
Kibaba kimoja mwenye umri wa
miaka 33 nchini Uganda ametiwa
korokoroni na polisi nchini Uganda
baada ya kujifanya yeye ni Waziri
wa mambo ya Nje wa Uganda Sam
Kutesa na kudai shilingi milioni 165
kwa muwekezaji mwenye asili ya
Kiasia.
Jamaa huyo mfanyabiashara kutoka
wilaya ya Wakiso mwenye umri wa
miaka 33 Collins kato, ambaye pia
hujulikana kwa jina la Moses
Barigye amekamatwa mjini Kololo
mjini Kampala na baadae
kukabidhiwa kwa mikononi mwa
polisi.
Kukamatwa kwa bw. Kato
kunafuatia malalamiko ya Vasavada
Asis mmiliki wa Kampuni ya Mara
Group iliyopo Kololo, ambaye
aliwataarifu maafisa usalama kuwa
Kato amekuwa akimbugudhi na
kudai fedha kutoka kwake.
Inadaiwa kuwa Bw. Kato alikuwa
akimwambia muwekezaji Asis kuwa
yeye kama Waziri anahitaji fedha
kwa ajili ya ziara ya kikazi nje ya
nchi kwenye mkutano wa kimataifa
na kuwa atailipa kwa
kumuunganishia mikataba poa ya za
serikalini.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi
wa Kampala Metropolitan Ibin
Ssenkumbi, mfanyabiashara huyo
aliingia kwenye mstari na kuwataka
wafanyakazi wake kuweka fedha
hizo kwenye mfuko na kumpelekea
Kato.
Lakini machale yaliwacheza baadhi
ya wafanyakazi hao waliokuwa na
namba ya simu ya Mh. Waziri
Kutesa na kuamua kumpigia na
kumuuliza fedha hizo tukuletee
wapi? Jambo lilimshtua na
kushangaa fedha na za nini tena
kutoka kwa naniii..???
Baada ya hayo taarifa ilifikishwa
polisi, ambapo sasa wao walijifanya
ni wafanyakazi wa Nara Group na
kuwa wakutane wamkabidhi fedha
zake, ambapo alipotia timu aliishia
kucheza na pingu na sasa anajuta
kujifanya waziri.
HUU NDO ULE UJUMBE ALIYOUANDIKA YULE KIJANA ALIYE JINYONGA DODOMA
Ujumbe ulioachwa na Oscar John
(24) mkazi wa mkoa wa Dodoma
aliyejinyonga hadi kufa baada ya
kuhisi amemuuwa mchumba wake
kwa kumkata kata kwa
kisu,umepatikana.
Oscar alijinyonga chumbani kwa
mchumba wake Maria Chilinde (25)
ambaye ni mfanyakazi wa chuo cha
VETA mjini Singida baada ya
kumkata kata kwa kutumia kisu.
Katika ujumbe huo, marehemu
Oscar aliandika 'mimi Oscar John
nimekufa pamoja na Maria,hela elfu
tisini pamoja na simu zangu
watachukua wazazi wangu.By by
wapendwa wote'.
Kwa mujibu wa mkuu wa chuo cha
VETA mjini Singida Afridon
Mukhomoi, marehemu Oscar
atakuwa ameandika ujumbe huo
baada ya kubaini amemuuwa Maria
na alipomaliza kuuandika,
alijitundika kwenye kenchi kwa
kutumia pazia na kusababisha kifo
chake.
Amesema kuwa wakati tukio hilo la
kusikitisha linatokea, yeye
hakuwepo lakini alielezwa kuwa
baada ya Maria kuzirai na Oscar
kuhisi kuwa amefariki dunia,
alimfunika kwa shuka na kuandika
ujumbe huo na
Marehemu Oscar inadaiwa
amefanya unyama huo baada ya
wazazi wa Maria kudai mahari ya
shilingi milioni mbili,ndipo aolewe
na Oscar.Oscar alishindwa kumudu
kiwango hicho na hivyo kuamua
wote wafe.
A BUSY NIGHT..
Spain face off against France,
Germany host Sweden, Italy welcome
Denmark and England travel to
Poland in a busy night of action
across Europe.
Follow me on twitter @hudo486 for all the latest news...
HILI NDO TAMKO LA WAISLAM LEO
Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
nchini Tanzania wametoa tamko
kufuatia kitendo cha kijana
Emmanuel Josefati (14) kukojelea
kitabu kitukufu cha Qur'an na
kusababisha mgongano wa mawazo
miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao
wamesema 'Tunalaani Kitendo cha
kukojolewa Qur'an Tukufu ambayo
ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam
Wote Duniani'.
'Tunataka kusikia tamko la serikali
la kulaani kitendo cha kukojolewa
Qur'an'.
'Tunataka serikali kukemea kitendo
cha Jeshi la Polisi kushambulia
Misikiti, waumini na Kuvuruga
ibada'.
'Tunalaani vitendo vya uchokozi wa
kidini'.
'Tunalaani matumizi ya matumizi ya
nguvu kubwa dhidi ya raia
yaliyofanywa na Polisi'.
'Tumehuzunishwa sana na kitendo
na kitendo cha kushambuliwa
Misikiti na Makanisa kilichotokea
Mbagala'.
'Tunatoa siku 7 ndani ya siku hizi
Waislamu wanaoshikiliwa na Polisi
wapewe haki yao ya dhamana'.