Naibu Waziri Philipho Mulugo.
Kuanzia juzi taarifa na video ya
Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo
ya ufundi wa Tanzania Philipo
Augustino Mulugo zimeanza
kusambaa kwa watanzania wengi
kuhusu alichosema akiwa Afrika
Kusini kwenye mkutano wa
kimataifa kwamba Tanzania ni
muungano wa visiwa vya bahari ya
Hindi, Pemba na Zimbabwe.
Mulugo leo amezungumza na Power
Breakfast ya CLOUDS FM na kusema
kabla ya yeye kupanda kuanza
kuzungumza kulikua na kiongozi wa
Zimbabwe ambae alitoka
kuzungumza na nina mkariri
akisema "sasa ilibidi lazima baada
ya kufika pale ni lazima umshukuru
mwenzako aliepita sasa kama
mawazo ndiyo yaliyokua
yamedhania hivyo kwamba basi
hapa naitamka Zimbabwe kwa
sababu zote zimeanzia na Z labda
ilitokea hivyo lakini nakiri kabisa
kwamba sikua na makusudio
kwamba naitamka Zimbabwe lakini
kule kwenye power presentation
inaonekana kabisa ukifungua pale
ni Tanzania imeungana na Zanzibar
Pemba na Tanganyika kama
ambavyo tunajua kwa sababu ile ni
historia hakuna asiejua hata mtoto
wa darasa la tatu"
"Niseme tu kwamba hiyo ni
kuteleza kwa ulimi na nilikua
namfikiria yule waziri wa Zimbabwe
kwa sababu alikua ametoka
kuhutubia kabla ya mimi, nilikua
naomba ieleweke hivyo………… na
wengi wameongea wanahoji lugha
kiingereza, jamani tukubaliane
kwamba kusema Zimbabwe badala
ya Zanzibar sidhani kama inaendana
na drama yenyewe kwa sababu
mimi nimekua mwalimu mda mrefu
nimefundisha wanafunzi wangu na
wananifahamu uwezo wangu
mkubwa na tena mimi ni mwalimu
wa historia hata degree yangu ni
mimi ni mwalimu wa historia na
Economics, labda niliongea nilikua
sijielewi na ningegundua
nimetamka Zimbabwe ningeweza
kuomba radhi, mataifa yote wawe
waafrika wawe wazungu wengi huwa
tunazingatia kuangalia kwenye
power point pale, wengi huwa
hawasikilizi sauti" – Mulugo
Kuhusu kukosea kutaja mwaka,
Namkariri naibu waziri akisema
"mimi pale nia yangu ilikua ni
kusoma namba moja moja
nikashtukia nakwenda kusoma
mbili, haijakaa kama nimekosea
kiingereza kama watu
wanavyoipanua kwa mfumo huo
lakini kama watu wamenielewa
hivyo niombe tu msamaha"
Thursday, October 25, 2012
HICHI NDO ALICHOSEMA NAIBU WAZIRI MULUGO KUHUSU KUSEMA TZ NI MUUNGANO WA ZIMBABWE NA PEMBA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment