Licha ya kuwepo kwa
malalamiko mengi kutoka kwa
wasanii wa filamu Bongo kuwa
wanapata maslahi kiduchu
kutoka katika kazi hiyo nguli wa
maingizo kupitia vichekesho King
Majuto ameanika hadharani
lundo ma mali alizovuna
kutokana na fani hiyo.
Aliojiwa na teentz.com juzi
kati Mzee Majuto alitanabaisha
kuwa licha ya kuwepo kwa
dhuluma nyingi kutoka kwa watu
wanajiita wadaau wa filamu
lakini amefanikiwa kuvuna
nyumba na magari kadhaa
kutoka katika kazi yake hiyo
aliyoifanya kwa miaka zaidi ya 35
sasa.
"Ni kweli haki zetu nyingi
zinapotea, lakini nashukuru
mungu kwa miaka zaidi ya 35
niliyofanya kazi ya uigizaji
nimefanikiwa kujenga nyumba
moja kubwa ambayo pia ina
sehemu kubwa ya wazi huku pia
nikifanikiwa kununua magari
mawili moja likiwa la kisasa pia
namiliki biashara kadhaa binafsi
na hivi karibuni nimefungua
kampuni yangu ya kurekodi
filamu" alisema Majuto
Story kutoka www.teentz.com
Tuesday, October 30, 2012
HUU NDO UTAJIRI WA KING MAJUTO BAADA YA KUKAA KWENYE GAME ZAID YA MIAKA 35
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment