Habari kutoka Kariakoo ameripoti kwamba makundi ya wananchi ambao wapo Kariakoo
yameanza kuondoka Kariakoo kuelekea majumbani kwa sababu hali sio
nzuri, polisi wametanda kwenye barabara zote ambapo magari yanayotoka
sehemu mbalimbali kuingia mjini yamezuiwa kuingia kutokana na kikundi
cha waandamanaji kilichojiandaa kuandamana kuelekea kwenye ofisi ya
Waziri mkuu kutawanyishwa kwa mabomu ya machozi na kikundi
kikasambaratika.
Polisi bado wanaendelea
kudumisha ulinzi ambapo kwa sasa maduka yamefungwa na mengine
yanaendelea kufungwa, shughuli nyingine za kawaida zimesimama na kwa
sasa msururu wa watu unarudi kuelekea majumbani, vikundi vya maandamano
vimeripotiwa kujikusanya kwenye maeneo tofauti tofauti.
Polisi wanatumia Farasi, Mbwa
na magari kusimamia amani ambapo vikundi vilivyojaribu kuandamana
vilikua na bendera na wengine walikua na fimbo kabisa, na walikua na
gari maalum ambalo walikua wamepanga ndio walitumie kwenda mjini kwenye
ofisi ya waziri mkuu lakini polisi wakawawahi na kuwasambaratisha.
No comments:
Post a Comment