Monday, October 22, 2012

AGIZO KUTOKA SEREKALINI KUHUSU MSG INAYOSAMBA KWA KUTISHO

Kuna taarifa kwenye mitandao ya
simu inayoendelea kutolewa
kwenye message za simu kwamba
kuna Mabomu zaidi ya 30 yenye
uzito usiopungua tani 100 na
kuwataka wananchi katika mikoa ya
Tanzania iliyo jirani na Malawi kuwa
waangalifu.
Taarifa hiyo imetaka wenye
wasiwasi kuhusu taarifa hiyo wapige
simu 0756000042. Taarifa hiyo
imedai kwamba imetolewa na Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Tunapenda kutoa taarifa kwamba
taarifa hizo siyo za kweli na lengo
lake haliwezi kuwa zuri kwa
Watanzania. Wananchi
wanashauriwa kutotuma taarifa
zozote kwenye namba hiyo ama
kuziamini taarifa za aina hiyo.
Imetolewa na

Assah Mwambene
Mkurugenzi, Idara ya Habari
Maelezo.

No comments:

Post a Comment