Jumuiya Ya Uamsho na
Mihadhara Ya Kiislamu Zanzibar
.....
Amesema kuwa waliomchukuwa
walijitambulisha kwake kuwa ni
askari polisi na kumonesha
vitambulisho huku wengine
wawili wakiwa na silaha za
mshingani hapo hapo
wakamfunga macho yake kwa
kutumia kitambaa ili asijue wapi
anapelekwa walimchukua kwa
gari na baadae kumuingiza katika
nyumba asioijua kwa mahojiano
bila ya kumfungua kitambaa
hicho kwa muda ...
wa siku tatu mfululizo.
Amesema kuwa watu hao
waliomuhoji maswala mengi
sana kuhusu tangu kuuanzishwa
kwa jumuia ya uamsho na safari
zake za kwenda omani na mpaka
kumchukulia simu yake bila ya
kumrejeshea pia wametaka kujua
kuwa anauhusiano gani na rais
shein na makamo wakwanza wa
raisi maalim seif, wakati
wanamuhoji walifika mpaka
kupiga risasi chini ya miguu nyake
ili kumtisha na kuweza kufikia
lengo lao walilojipangia.
Amesema pia watu
waliomchukuwa na baadhi ya
waliokuwa wanamlinda hawezi
kuwajua kutokana na kuwa
walikuwa wamevaa soksi ndani ya
nyuso zao nakubakisha macho
tu,amsema kutokana tu na lafdhi
zao ambazo walikuwa
wanaongea inaonekana wazi
kuwa wengi ni kutoka bara na
wazanzibari ni kama wawili tu
kutokana na sauti zao.
kuhusu suala lakupigiwa simu na
mtu asiemjua amesena kuwa
wao kama viongozi huwa mara
nyingi wamekuwa wakipigiwa
simu na watu wasiowajua na
wamekuwa wakionanan nao bila
ya matatizo hivyo basi kitendo
cha kupigiwa simu siku hio na
mtu asiemjua hakikumshituwwa
kwani nikawaida kwao hususani
aliemnigia alijitambulisha kama ni
mwanafunzi wake wa mahad
lmahfudh
Aidha amesema kuwa muda
wote huo wa siku tatu hakuweza
kula chochote katika chumba
hicho kwani alikuwa hawaamini
na badala yake alikuwa
anakunywa maji kutoka bomba la
mfereji lililokuwa chooni katika
chumba hicho pia amesema
wakati yupo ndani hakujua lolote
linaloendelea huku nje isipokuwa
amejua baada ya kutoka nje kwa
kuambiwa na kila manaemkuta.
Aidha sheikh farid ameiomba
serikali ya mapinduzi ya zanzibar
kutumuia sheria na uadilifu kwa
rai wake kinyume cha hivo
watakuwa wanaimba tu katika
nchi amani na utulivu
usiokuwepo pia amewataka
wazanzibar kuendelea kutetea
maslahi ya nchi yao kama
kawaida kwani kufanya hivo ni
haki yao na yeye amewahakikishi
ataendelea kuitetea zanzibar
mpaka tone la mwisho la damu
yae.
Saturday, October 20, 2012
HUU NDO MKASA MZIMA WA KUTEKWA KWA SHEIKH FARIDI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment