Kibaba kimoja mwenye umri wa
  miaka 33 nchini Uganda ametiwa
  korokoroni na polisi nchini Uganda
  baada ya kujifanya yeye ni Waziri
  wa mambo ya Nje wa Uganda Sam
  Kutesa na kudai shilingi milioni 165
  kwa muwekezaji mwenye asili ya
  Kiasia.
  Jamaa huyo mfanyabiashara kutoka
  wilaya ya Wakiso mwenye umri wa
  miaka 33 Collins kato, ambaye pia
  hujulikana kwa jina la Moses
  Barigye amekamatwa mjini Kololo
  mjini Kampala na baadae
  kukabidhiwa kwa mikononi mwa
  polisi.
  Kukamatwa kwa bw. Kato
  kunafuatia malalamiko ya Vasavada
  Asis mmiliki wa Kampuni ya Mara
  Group iliyopo Kololo, ambaye
  aliwataarifu maafisa usalama kuwa
  Kato amekuwa akimbugudhi na
  kudai fedha kutoka kwake.
  Inadaiwa kuwa Bw. Kato alikuwa
  akimwambia muwekezaji Asis kuwa
  yeye kama Waziri anahitaji fedha
  kwa ajili ya ziara ya kikazi nje ya
  nchi kwenye mkutano wa kimataifa
  na kuwa atailipa kwa
  kumuunganishia mikataba poa ya za
  serikalini.
  Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi
  wa Kampala Metropolitan Ibin
  Ssenkumbi, mfanyabiashara huyo
  aliingia kwenye mstari na kuwataka
  wafanyakazi wake kuweka fedha
  hizo kwenye mfuko na kumpelekea
  Kato.
  Lakini machale yaliwacheza baadhi
  ya wafanyakazi hao waliokuwa na
  namba ya simu ya Mh. Waziri
  Kutesa na kuamua kumpigia na
  kumuuliza fedha hizo tukuletee
  wapi? Jambo lilimshtua na
  kushangaa fedha na za nini tena
  kutoka kwa naniii..???
  Baada ya hayo taarifa ilifikishwa
  polisi, ambapo sasa wao walijifanya
  ni wafanyakazi wa Nara Group na
  kuwa wakutane wamkabidhi fedha
  zake, ambapo alipotia timu aliishia
  kucheza na pingu na sasa anajuta
  kujifanya waziri.
Tuesday, October 16, 2012
HII IMETOKEA UGANDA, KIBABA KIMEJIFANYA WAZIRI WA MAMBO YA NJE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment