Tuesday, October 16, 2012

HUU NDO ULE UJUMBE ALIYOUANDIKA YULE KIJANA ALIYE JINYONGA DODOMA

Ujumbe ulioachwa na Oscar John
(24) mkazi wa mkoa wa Dodoma
aliyejinyonga hadi kufa baada ya
kuhisi amemuuwa mchumba wake
kwa kumkata kata kwa
kisu,umepatikana.
Oscar alijinyonga chumbani kwa
mchumba wake Maria Chilinde (25)
ambaye ni mfanyakazi wa chuo cha
VETA mjini Singida baada ya
kumkata kata kwa kutumia kisu.
Katika ujumbe huo, marehemu
Oscar aliandika 'mimi Oscar John
nimekufa pamoja na Maria,hela elfu
tisini pamoja na simu zangu
watachukua wazazi wangu.By by
wapendwa wote'.
Kwa mujibu wa mkuu wa chuo cha
VETA mjini Singida Afridon
Mukhomoi, marehemu Oscar
atakuwa ameandika ujumbe huo
baada ya kubaini amemuuwa Maria
na alipomaliza kuuandika,
alijitundika kwenye kenchi kwa
kutumia pazia na kusababisha kifo
chake.
Amesema kuwa wakati tukio hilo la
kusikitisha linatokea, yeye
hakuwepo lakini alielezwa kuwa
baada ya Maria kuzirai na Oscar
kuhisi kuwa amefariki dunia,
alimfunika kwa shuka na kuandika
ujumbe huo na
Marehemu Oscar inadaiwa
amefanya unyama huo baada ya
wazazi wa Maria kudai mahari ya
shilingi milioni mbili,ndipo aolewe
na Oscar.Oscar alishindwa kumudu
kiwango hicho na hivyo kuamua
wote wafe.

No comments:

Post a Comment