Taasisi na Jumuiya za Kiislamu
nchini Tanzania wametoa tamko
kufuatia kitendo cha kijana
Emmanuel Josefati (14) kukojelea
kitabu kitukufu cha Qur'an na
kusababisha mgongano wa mawazo
miongoni mwa watanzania.
Katika tamko lao
wamesema 'Tunalaani Kitendo cha
kukojolewa Qur'an Tukufu ambayo
ni Kitabu Kitakatifu kwa Waislam
Wote Duniani'.
'Tunataka kusikia tamko la serikali
la kulaani kitendo cha kukojolewa
Qur'an'.
'Tunataka serikali kukemea kitendo
cha Jeshi la Polisi kushambulia
Misikiti, waumini na Kuvuruga
ibada'.
'Tunalaani vitendo vya uchokozi wa
kidini'.
'Tunalaani matumizi ya matumizi ya
nguvu kubwa dhidi ya raia
yaliyofanywa na Polisi'.
'Tumehuzunishwa sana na kitendo
na kitendo cha kushambuliwa
Misikiti na Makanisa kilichotokea
Mbagala'.
'Tunatoa siku 7 ndani ya siku hizi
Waislamu wanaoshikiliwa na Polisi
wapewe haki yao ya dhamana'.
Tuesday, October 16, 2012
HILI NDO TAMKO LA WAISLAM LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment