SIMBA YAIVA COASTAL UNION YA TANGA BILA YA NGASA, OKWI NA REDONDO.
KLABU ya soka ya Simba inatarajia kuwakosa wachezaji wake hao nyota katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga Kesho Jumamosi.
Wachezaji watakaokosa mchezo huo utakaopigwa katika Uwanja wa Mkwakwani ni pamoja na Mrisho Ngassa na Ramadhani Chombo “Ridondo” ambao wanasumbuliwa na malaria, Haruna Shamte anayesumbuliwa na enka pamoja na Kiggi Makassi anayesumbuliwa na goti. Wengine ni Emmanuel Okwi aliyeitwa katika timu yake ya taifa ya Uganda, Abdallah Seseme na Wazir Hamad. Wachezaji ambao watasafiri na timu hiyo ni pamoja na makipa Juma Kaseja, Wilbert Mweta mabeki ni Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman Keita. Viungo ni Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban akati washambuliaji watakuwa Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.
MAKIPA:Juma Kaseja na Wilbert Mweta.
Walinzi: Chollo, Maftah, Nyoso, Paschal Ochieng, Kapombe, Hassan Khatib, Paulo Ngalema, Koman Keita.
Viungo: Kazimoto, Jonas Mkude, Kiemba, Salim Kinje, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Boban.
Washambuliaji:Sunzu, Edward Christopher, Haroun Chanongo, Daniel Akuffo na Abdallah Juma.
RATIBA RAUNDI YA 7
13.10.2012. | 45 | POLISI MOROGORO | vs AZAM | JAMUHURI | MOROGORO | |
13.10.2012. | 46 | TANZANIA PRISONS | vs JKT OLJORO | SOKOINE | MBEYA | |
13.10.2012. | 47 | COASTAL UNION | vs SIMBA | MKWAKWANI | TANGA | |
13.10.2012. | 48 | RUVU SHOOTINGS vs | AFRICAN LYON | MABATINI | PWANI | |
13.10.2012. | 49 | MTIBWA SUGAR vs | MGAMBO JKT | MANUNGU | MOROGORO |
No comments:
Post a Comment