Inasemekana kufa kwa nyangumi huyu kumepelekea sehemu
kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi
mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza
kushambuliwa na jamii ya papa weupe.
Mzoga
wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa
ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza
kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.
Mamlaka
husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga
mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari.
|
No comments:
Post a Comment