KIJANA aliyewahi kupata umaarufu mkubwa nchini kwa jina la Rama ‘mla
watu’, Ramadhan Seleman anayetuhumiwa kwa kosa la mauaji baada ya
kukutwa na kichwa cha mtoto, Salome Yohana (3) mwaka 2008, amepelekwa
Hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma, kupimwa akili. Habari kutoka
Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam zinasema kuwa mtuhumiwa huyo
amepelekwa Mirembe ili kufanyiwa uchunguzi wa akili yake. Akizungumza
na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini, afisa mmoja
wa Jeshi la Magereza Kanda ya Dar es Salaam amesema wamelazimika
kumpeleka Rama katika hospitali hiyo ya akili kutokana na vituko vyake.
“Tumeona
ni heri tumfanyie uchunguzi wa akili kwa sababu ilikuwa ni vigumu
kuendelea na kesi mahakamani kutokana na vituko alivyokuwa akivifanya
tangu alipokamatwa. “Miongoni mwa mambo yanayotatanisha ni pale
alipokamatwa akiwa anakula kichwa cha mtu, hicho siyo kitu cha kawaida,
hivyo ni muhimu kumchunguza akili yake kwanza. |
No comments:
Post a Comment