Ni binti mwenye mikono yote
miwili,Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Alfa
Germ, Morogoro, Jessica Kiliani (17), amefanya mtihani wa kuhitimu
kidato cha nne akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji kwa zaidi ya
masaa mawili na madaktari!
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Jessica
kuomba aruhusiwe kufanya mtihani huo licha ya kuwa wodini akiugua
kufuatia operesheni aliyofanyiwa na kulazwa katika wodi ya wazazi namba
7B.
Mama mzazi wa Jessica, Anna Ngapemba alisema alipigiwa simu
na mkuu wa shule saa 6:00 usiku Jumamosi iliyopita akimjulisha kuwa
binti yake anasumbuliwa na tumbo na anahitaji msaada wa haraka. Mama wa
Jessica alisema alienda shuleni hapo usiku huohuo na kukutana na mama
mlezi (matron) wa hosteli za shule hiyo na kujulishwa juu ya hali ya
binti yake na kwa kushirikiana na uongozi wa shule hiyo, walimpeleka
katika Hospitali ya Mkoa.
Alisema wauguzi waliokuwa hospitali
usiku huo walimpigia simu daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake,
Christopher Manumbu. Dr Manumbu alipofika hospitalini hapo, alimfanyia
Jessica upasuaji haraka kutokana na hali yake kuwa mbaya.
Jessica
licha ya kuwa katika hali ya maumivu alifanya mitihani miwili
(Kiingereza na uraia) kama wenzake, katika wodi hiyo ya wazazi, akiwa
chini ya msimamizi wa mitihani na polisi,
Jessica alisema hakuwa
tayari kuikosa mitihani hiyo na ndiyo maana alimwomba mama yake
kuwasiliana na uongozi wa shule yake ili umwandalie mazingira mazuri ya
kufanya mtihani akiwa wodini.
Mungu ambariki msichana huyu afaulu mitihani kusema kweli ameonesha ujasir wa khali ya juu.
No comments:
Post a Comment